Thursday, November 4, 2010

MGOMBEA CHADEMA AZIRAI TARIME BAADA YA KUSOMEWA MATOKEO.


HATIMAYE Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kutwaa jimbo la Tarime ambalo lilikuwa likishikiliwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa miaka mitano,huku mgombea wa CHADEMA, Mwita Mwikwabe akiangua kilio hadi kuzirai. Mgombea huyo alizirai baada ya matokeo kuhesabiwa tena na kubaini kuwa ameshindwa ,ambapo mgombea wa CCM, ambaye ni mtunzi wa vitabu, Nyabari Nyangwine,amefanikiwa kushinda kwa tafauti ya kura 730.
Akitangaza mataokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Tarime, Fedelis Lumato,alisema kuwa Mgombea wa CCM,Nyambari Nyangwine ameshinda kwa kura 28,064 huku mgombea wa Chadema Mwita Mwikwabe akipata kura 27334 ambapo aliyekuwa anatetea kiti hicho Charles Mwera wa CUF akiambulia kura 7368.
Lumato alisema kuwa mgombea wa NCCR-Mageuzi ,Peter Wangwe amepata kura 7811,mgombea wa UDP, Mchungaji Jacob Mwita ameambulia kura 185 akifuatiwa na mgombea wa TLP ambaye ni mwandishi wa habari na Mwanasheria Kichere Nyaronyo aliyepata kura 45 tu.
Aidha CCM imefanikiwa kutwaa halmashauri hiyo baada ya kupata madiwani 17 dhidi ya Chadema waliopata madiwani 12 na CUF wakiambulia kiti kimoja kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Mwera aliyepewa aliyepata kujifariji.
Kwa upande wa matokeo ya Rais Mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, amepata kura 34930 sawa na asilimia 49 dhidi ya Mgombea wa Chadema 32470 sawa na asilimia 46 huku akifuatiwa na mgombea wa CUF aliyepata kura 1804 na mgombea wa APPT-Maendeleo Piter Kuga Maziray akiambulia kura 889sawa na asilimia 1.3.

MGOMBEA WA CHADEMA JIMBO LA TARIME MWITA MWIKWABE AKIANGUA KILIO HUKU AKISAIDIWA NA MENEJA KAMPENI WAKE KINYANGA.

No comments: