Thursday, November 4, 2010

Kikwete mambo safi

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ameendelea kuongoza katika matokeo rasmi ya urais yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambapo hadi sasa anaongoza katika majimbo 145.

Hadi jana jioni NEC ilikuwa imetangaza matokeo ya urais katika majimbo 171 kati ya 239 yaliyopo.

Matokeo hayo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Lewis Makame kwa kushirikiana na Makamu wake, Jaji Omar Makungu, yanaonesha aliyeshika nafasi ya pili ni mgombea wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amenyakua majimbo 19.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa kwa siku tatu mfululizo imebainika kuwa mgombea wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa anaongoza katika majimbo saba na yote ni ya Tanzania Bara.

Majimbo anayoongoza Kikwete ni Arumeru Magharibi, Bunda, Busega, Dodoma Mjini, Ilala, Kibakwe, Kigoma Kusini, Lupa, Magu Mjini, Mbinga Magharibi, Mbozi Mashariki, Mpwapwa na Mvomero.

Mengine ni Mwibara, Sengerema, Serengeti, Singida Kaskazini, Singida Magharibi, Singida Mashariki, Sumbawanga Mjini, Sumve, Temeke, Ukonga, Urambo Mashariki, Bukoba Vijijini, Chaani, Chalinze, Chwaka, Fuoni, Handeni, Iramba Magharibi, Kalenga, Kigoma Mjini, Kikwajuni, Kilindi, Kyela, Liwale, Lushoto, Mfenesini, Misungwi na Moshi Vijijini.

Yamo pia ya Mpanda Vijijini, Mtwara Vijijini, Musoma Vijijini, Nzega, Rungwe Magharibi, Rungwe Mashariki, Tunduru Kaskazini, Ulanga Mashariki, Buyungu, Dimani, Dole, Donge na Kalambo.

Mengine ni Kigoma Kaskazini, Kisarawe, Kisesa, Kishapu, Kwela, Manyoni Magharibi, Manyoni Mashariki, Matemwe, Mkwajuni, Mwanakwerekwe, Nungwi, Kigamboni, Tumbatu, Arumeru Mashariki, Buchosa, Igalula, Kondoa Kusini, Mbarali, Muleba Kaskazini, Njombe Kaskazini, Tabora Kaskazini na Tunduru Kusini.

Majimbo mengine ‘ya Kikwete’ ni Amani, Bagamoyo, Bububu, Bumbwini, Chumbuni, Igunga, Jang’ombe, Katavi, Kiteto, Kitope, Kwahani, Kwamtipura, Lindi Mjini, Mafia, Magomeni, Mchinga, Meatu na Mkinga.

Mengine ni Monduli, Mpendae, Mtama, Mtera, Mufindi Kaskazini, Mufindi Kusini, Ngorongoro, Pangani, Peramiho, Rahaleo, Ruangwa, Simanjiro na Tanga Mjini. Pia Biharamulo Magharibi, Busanda, Geita, Hai, Ileje, Iramba Mashariki, Ismani, Iringa Mjini, Kibaha Vijijini, Kilolo, Kondoa Kaskazini, Kongwa na Korogwe Vijijini.

Kadhalika Ludewa, Mkuranga, Mwanga, Nkasi Kusini, Nkasi Kaskazini, Newala, Nyang’wale, Nyamagana, Nkenge, Nachingwea na Same Mashariki, Same Magharibi, Sikonge, Songea Mjini, Songwe na Ulanga Mashariki. Pia Singida Mjini, Korogwe Mjini, Njombe Kusini, Babati Mjini, Mtwara Mjini, Longido, Chilonwa, Mpanda Vijijini na Siha.

Majimbo anayoongoza Profesa Lipumba ni Chake Chake, Mtoni, Micheweni, Konde, Tumbe, Mgogoni, Ziwani, Chambani, Chonga, Gando, Kiwani, Kojani, Mji Mkongwe, Mkanyageni, Mkoani, Mtambile, Mtambe, Wawi na Wete. Dk. Slaa anaongoza katika majimbo sita ya Arusha Mjini, Ilemela, Bukoba Mjini, Mbeya Mjini, Moshi Vijijini, Musoma Mjini na Babati Vijijini.

Mbali na wagombea hao watatu walioongoza katika majimbo, wagombea wengine walioshiriki kinyang’anyiro hicho ambao hawajaongoza katika jumla ya kura za majimbo ni wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray; Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi, Mutamwega Mgahywa wa TLP na Fahmi Dovutwa wa UPDP.

No comments: