
Ikilinganishwa na uchaguzi uliokwisha 2005, ambapop upinzani Bara walipata viti 6 pekee na Zanzibar viti 19, mwaka huu 2010 wapinzani wamefanikiwa kunyakua majimbo mengi zaidi (23 Bara, 3 Zanzibar).
Kinana amesema ongezeko hilo linatokana na kukua kwa demokrasia na vile vile akagusia kuwa, huenda hatua za CCM za kukemea vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watu walioonesha nia ya kuwania nyadhifa za uwakilishi kupitia chama hicho, kilichochea kuundwa kwa makundi, jambo ambalo huenda likawa limechangia kwa wao kuanguka katika baadhi ya majimbo. Akasema vile vile kuwa MwanaCCM yeyote ambaye anadhani hakutendewa haki katika matokeo ya uchaguzi huu na akataka msaada, basi CCM itakuwa tayari kumsaidia.
Amemaliza kwa kuwapongeza Wazanzibari kwa mwenendo mzima wa uchaguzi na kwa ushindi walioupata.
from: http://www.wavuti.com
No comments:
Post a Comment