TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
YAH: KUAHIRISHA BAADHI YA CHAGUZI MBALIMBALI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.
Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-
1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa Zanzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)
2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:-
Na.
HALMASHAURI KATA
1 Newala DC Mtonya
2 Mbulu DC Endegikot
3 Manyoni DC Kitaraka
4 Same DC Kisiwani
5 Kibaha DC Janga
6 Rufiji (a)Kibiti
(b) Chemchem
(c) Ngorongo
(d) Kipugira
(e) Mjawa
7 Uyui DC (a)KIgwa
(b)Ibelamilundi
8 Sikonge Kisanga
9 Njombe Mji Mwema
10 Ulanga DC Msogezi
11 Karagwe DC (a) Kimuli
(b) Kamuli
12 Kasulu Kitagata
13 Chato DC Buseresere
14 Mwanza (Jiji) (a) Mkuyuni
(b) Mirongo
Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Madiwani utanaendelea kufanyika leo kama ilivyopangwa.
Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.
(Rajabu R. Kiravu)
Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi
No comments:
Post a Comment