Monday, November 1, 2010

Kura zinahesabiwa nchini Tanzania

Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea nchini Tanzania siku moja tu baada ya uchaguzi mkuu ambao ulikuwa na msisimuko mkali kuwahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi nchini humo miaka ya tisini.
atokeo ya mwanzo yanatarajiwa siku ya jumatano.

rais wa sasa Jakaya Kikwete amesema anatarajiwa kuhifadhi kiti hicho cha urais.

Kikwete alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Willibrod Sla ambaye alitumia muda wake mwingi wakati wa kampeini kupinga ufisadi.
Wafuasi wa chama cha CUF

Wafuasi wa chama cha CUF

Chama tawala cha Mapinduzi CCM, ambacho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo kujinyakulia uhuru wake, ilikabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama kadhaa vya kisiasa, kufuatia kudidimia kwa umaarufu wa serikali kutokana na madai ya ufisadi.

Kura kadhaa za maoni zimebainisha kuwa Rais Kikwete huenda akashinda muhula mwingine kama rais wa nchin hiyo.

Hata hivyo kura nyingine ya maoni ilionyesha kuwa mpinzani wa rais Kikwete Wilbord Slaa wa chama cha Party Of Democrasy and development CHADEMA alikuwa akiongea japo kwa kiasi kidogo sana.

No comments: