Saturday, June 11, 2011

BHOKE AWAJIBU WATANZANIA, ASEMA "WHAT'S THE BIG DEAL?"


Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa Amplified, Bhoke Egina, 26, ameamua kuwajibu watanzania kwa kutoa ujumbe mkali katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii (Facebook).

Bhoke, aliyetupwa nje ya shindano hilo Jumapili iliyopita, alifanya mapenzi waziwazi na aliyekuwa mshiriki wa Uganda, Ernest Wasake, 28, wakiwa kwenye shindano hilo huku wakirekodiwa na kamera za BBA.

Bhoke ameandika maneno haya "What's the big deal? People were just making a lot of noise about the whole issue as if we were having sex on the street. BBA Amplified house is for adults and whoever cannot 'suck it' up should not even be watching."

Licha ya kuandika maneno hayo alidiriki kusema kwa kinywa chake mwenyewe katika mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha Jahazi kinachorushwa na Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam alisema kuwa hakuna kitu chochote ambacho anajutia katika yale yote ambayo ameyafanya "Sijutii chochote, i really enjoyed being in the house na yote niliyoyafanya niliyafanya kama mimi hivyo hakuna chochote ambacho naweza nikajutia..."

No comments: