Tuesday, May 24, 2011

KWA WAPENZI WA MIELEKA..'MACHO MAN' AMEFARIKI DUNIA

Mmoja wa wakali wa mileleka duniani Randy Savage a.ka Macho Man amefariki dunia akiwa na miaka 58,kwa ajali ya gari huko Seminole,Florida-Marekani baada ya kupata ghafla ugonjwa wa moyo wakati akiendesha gari....
Randy Savage au Macho Man alianza mchezo wa mieleka mwaka 1985 kupitia WWF na alijulikana sana kwa msemo wake wa "Ooooooh Yeaahhhhh" ulingoni
Wakati anapata ajali alikua anaendesha gari aina ya Jeep Wrangler na aligonga mti ghafla, baada ya hapo alikimbizwa Largo Medical Center kwa matibabu lakini alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.
R.I.P Randy Savage a.k.a Macho man.

No comments: