SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.
Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.
“Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,” amesema Mufti Simba leo.
Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.
Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.
“Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja” alisema Mufti Simba.
Amelaani mashambulizi ya baadhi ya Magharibi dhidi Libya, akisema kinaonesha ile ni vita dhidi ya Uislamu na siyo vinginevyo kwa kuwa ni kawaida ya nchi ya Marekani kuziandama nchi zenye Waislamu.
Kuhusu Mahakama ya Kadhi, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wake kwa kuwa ni moja ya nguzo muhimu ndani ya dini hiyo huku pia akiwataka maaskofu kuacha kuingilia kati suala hilo.
Ameshangazwa kuona Waislamu wanapotaka kufanyiwa jambo lolote kunajitokeza ugumu kulitekeleza tofauti na dini nyingine, jambo alilosema halipaswi kufanywa hivyo kwa kuwa ‘wote ni watoto wa baba mmoja.’
source:HABARI LEO
1 comment:
… Unbelievable , but I just found software which can do all hard work promoting your atmbeya.blogspot.com website on complete autopilot - building backlinks and getting your website on top of Google and other search engines 1st pages, so your site finally can get laser targeted qualified traffic, and so you can get lot more visitors for your website.
YEP, that’s right, there’s this little known website which shows you how to get to the top 10 of Google and other search engines guaranteed.
I used it and in just 7 days… got floods of traffic to my site...
…Well check out the incredible results for yourself -
http://autopilot-traffic-software.com
I’m not trying to be rude here, but I believe when you find something that finally works you should share it…
…so that’s what I’m doing today, sharing it with you:
http://autopilot-traffic-software.com
Take care - your friend George
Post a Comment