Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM wamegoma kuingia madarasani wakipinga kile walichodai kuwa ni hatua ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini kuchelewesha mikopo wanayostahili kupata.Polisi mkoani Dodoma wamelazimika kutumia nguvu za ziada kuwatawanya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma,UDOM waliokuwa wanaandamana kwenda ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kuwasilisha madai yao.
Dokta Nsekela amewataka wanafunzi hao kuwasilisha hati za madai yao katika ofisi yake na kuahidi kulitatua tatizo hilo ndani ya muda wa siku saba.
Hatua hiyo inafuatia juhudi za Mkuu wa Mkoa huo, DR James Msekela kuwasihi kutawanyika kwa amani wakati madai yao ya fedha za mafunzo kwa vitendo yakifanyiwa kazi kushindikana.
Mambo yalianza taratibu wakati wanafunzi hawa walipoamua kuziba barabara kuu inayoingia Chuoni kwao, UDOM.
Lengo lao la kutaka kuandamana hadi ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma ili kuwasilisha madai yao yakagonga ukuta, Askari polisi wenye silaha wakawazuia kwa muda huku Mkuu wa Mkoa Dr.James Alex Msekela akifanya juhudi za ziada kuwasiliana na Waziri Mkuu kuelezea hali hiyo ili kupata ufumbuzi.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa kuwa madai yao yameafikiwa na Waziri Mkuu ikapokelewa kwa hisia tofauti na kundi hilo la wanachuo.
Baada ya juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa kugonga mwamba, FFU wakatoa tangazo lenye kila tahadhari. Maandamano haya ni ya kwanza kufanyika chuoni hapa ikiwa ni wiki chache baada ya kuzinduliwa rasmi kwa chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM.
No comments:
Post a Comment