Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU mkoani Mbeya, imewakamata na kuwahoji madiwani kumi mkoani humo kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa uchaguzi wa mwenyekiti wa wilaya ya Chunya.
Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo Daniel Mkuta amethibitisha kukamatwa na kuhojiwa kwa madiwani hao ambao ni kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.
Hatua hiyo inakuja wakati wa harakati za chaguzi wa Mwenyekiti wa wilaya hiyo, unaofanyika hii leo Jumatano.
Madiwani hao ni wapiga kura katika uchaguzi wa ndani wa CCM katika uteuzi wa jina la mgombea wa chama hicho katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chunya.
No comments:
Post a Comment