Wednesday, November 3, 2010

CCM yazoa majimbo mengi ikifuatiwa na CHADEMA

Wakati Matokeo zaidi ya ubunge yakiendelea kutoka mpaka sasa matokeo yameshatangazwa katika majimbo 104 kati ya majimbo ya uchaguzi 239 nchini kote . Bado matokeo hayatangazwa katika majimbo 135.

Kati ya majimbo yaliyotangazwa matokeo, Chama cha Mapinduzi – CCM-kimepata ushindi katika majimbo 66, wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimepata viti 19, Chama cha Wananchi-CUF- kimeshapata viti 15, NCCR Mageuzi viti viwili na TLP viti viwili.Kumekuwapo na ucheleweshaji wa kutangazwa kwa matokeo katika baadhi ya majimbo kutokana na sababu mbalimbali mojawapo ukiwa ni pamoja na mpango wa Tume ya Taifa ya uchaguzi kutaka matokeo hayo kuingizwa kwenye compyuta ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kabla ya kutangazwa.

Matokeo ya hivi karibuni yametoka katika majimbo ya Kalenga na Makete ambapo katika majimbo hayo mawili wagombea wa Chama cha Mapinduzi walipata ushindi mkubwa. Dakta William Mgimwa wa jimbo la Kalenga alipata kura 31,421 wakati Dakta Binilith Mahenge wa jimbo la Makete alipata kura 22,290.

Katika jimbo la Bukombe huko Shinyanga Profesa Kayigela Kahigi ambaye alikuwa mgombea wa Chadema amepata ushindi kwa kura 19035.

Wakatihuohuo CCM yawataka wanachama wake kuchukua fomu za Uspika





Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake wanaotaka kuwania nafasi ya uspika wa bunge la muungano na lile la wawakilishi wa Zanzibar kuchukua fomu za maombi ya nafasi hiyo.

Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi, Luteni Yusuf Makamba amesema kwa wale ambao wangependa kugombea nafasi hiyo warejeshe fomu hizo siku ya taraehe nane Mwezi huu saa kumi jioni.

No comments: