Thursday, February 16, 2012

The Vibe club yawaangusha wapenzi wake

kwa mara nyingine jana Club pendwa ya jiji la mbeya(the vibe) iliwaangusha wadau wake pale ilipo ahirisha /kukatiza ile siku pendwa kwa wazee wa bakulutu(usiku wa mwambao)..habari zilizotufikia toka kwa wadau wengi ni ile hali ya kuwa kulikuwa na mpira wa kuvutia sana(arsenal Vs Ac Millan) ambapo wadau wa arsenal walitegemea kupunguzia maumivu yao kwa kulisakata rumba ndani ya club hiyo(maana walijua hawatatoka mbele ya ac millan)..

mwandishi wa blog hii alipopata taarifa alitembelea mahala hapo (the Vibe Out door)na kukuta wadau wengi wakilalamikia uamuzi wa club hiyo.hasa wakisema kwanini haikutangazwa mapema..na inasemekana redio inayomilikiwa na club ilikuwa inatangaza kuwa usiku wa mwambao utakuwa kama kawa...


Wadau wakiwa hawaamini nini kinaendelea...............

Stive...AKA King Mswati.."na leo kulikuwa na mpira muhimu sana...sasa baada ya mpira twende wapi???????????i hate it kwa kweli".



Samwel Majani anasema ..."sasa club inaendeshwagwa hivyo?mmenipotezea ratiba sana nilikuwa na wageni wangu kama kumi hivi na nilishawapromise nitawapeleka The vibe......yaniii mpaka jioni hii ndo najua kuwa hakuna ........club haiendeshwi kama soko jamaniii">>>

No comments: