Monday, January 16, 2012

MH TEMBA: NYOTA ILIYOZUNGUKWA NA WINGU

Alitangaza nia mapema, akachafuliwa, akajitoa, lakini ameongoza vema kampeni za Nicolas. Anaitwa Temba Francis, wengi humwita the Mastermind. Ni kijana mdogo sana mwenye umri usiozidi miaka 21 lakini hakika amekua jinamizi la kisiasa hasa kwa wagombea urais kutoka SOPAM na LAW.

Amekwishashika nyadhfa mbalimbali hata kabla ya kujiunga na chuo kikuu Mzumbe, na alikua naibu waziri wa mambo ya nje katika serikali ya Mh Uswege. Hivi karibuni alichaguliwa kuwa President Elect wa Mzumbe Rotaract Club.

Temba ni miongoni mwa watu wachache ambao wana mwonekano wa kiuongozi na kiutendaji. Maamuzi yake ya kujitoa katika mchakato wa Urais yaliwanyong'onyesha wengi na huenda pengo lake katika serikali ijayo likasababisha mapungufu makubwa.

Lakini kwa nini kinara huyu anakubalika sana na watu? Temba hakujaliwa sifa ya unafiki kama walivyo viongozi wengine wengi. Wachambuzi yakinifu wa mambo haya wanabainisha kuwa Temba is a Realistic leader. Wengi wamemfananisha na John F Kennedy.

Tunangoja kuona kijana huyu ametuandalia nini wana Mzumbe mwaka huu!

IMEANDIKWA na KRANTZ MWANTEPELE

No comments: