Friday, December 9, 2011

Uswazi Mr Ebbo



hii ndio VIDEO ya mwisho MR EBBO kuifanya, aliirekodi mwanzoni mwa mwaka huu na alikua na mpango wa kuitoa lakini ikashindikana kutokana na kuzidiwa Gafla, hivyo matibabu yakachukua nafasi kubwa zaidi.

hii inakua VIDEO ya KUMBUKUMBU kwa wakazi wote wa TANGA na TZ kwa ujumla, kwa sababu kati ya wanaoonekana ndani yake, sio MR EBBO peke yake aliofariki dunia, kuna rafiki yake mkubwa pia alishiriki lakini akafariki dunia siku chache tu baada ya video kumalizika, anaitwa CASSIM, alifariki dunia baada ya kugongwa na kusagwa na kiberenge maarufu kama TRENI ndogo, huyo jamaa aliyefariki yuko kwenye dakika ya pili kamili mpaka na sekunde saba, kavaa shati na suruali vinafanana rangi anatembea na baadae anaongea kama na fundi baiskeli.

JINGINE: video inapoanza wameandika STRICTLY NO MAKE UP, hilo lilikua agizo la MR EBBO mwenyewe kwa sababu ni video ya uswazi, akasema iandikwe hivyo kwamba MAKE UP hazihusiki kabisa, ni video ambayo hakuifanya mbali na anapoishi, kama kawaida watoto kibao walikusanyika manake walikua wanampenda sana.

No comments: