Tuesday, October 11, 2011

Mbeya yazidi kuchanuka.................JIJI la Kondoro


Benki ya Diamond Trust (T) Limited, imeendelea na mpango wake wa kusogeza huduma zao za kibenki karibu na Watanzania baada ya hivi karibuni kufungua tawi lake jijini Mbeya.

Kufunguliwa kwa huduma za benki hiyo katika jiji la Mbeya, kunaifanya benki hiyo kufikisha jumla ya matawi 13 katika sehemu mbalimbali za nchi, huku ikitarajiwa kufikisha matawi 15 hadi mwishoni mwa mwaka huu kwa kufungua mawili zaidi moja likiwa jijini Dar es salaam na jingine mjini Moshi.

Benki hiyo ambayo ina malengo ya kuwa benki bora zaidi katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara, ni miongoni mwa benki ambazo zimekuwepo nchini kwa muda mrefu kiasi lakini ikawa ikitoa huduma zake jijini Dar es salaam zaidi na kufunguliwa kwa tawi lake jijini Mbeya kunatarajiwa kuwarahisishia wakazi wa mji huo na hususan wajasiriamali wa kada zote, huduma za uwekaji na utoaji wa fedha pindi wanapokuwa kwenye safari zao za kibiashara baina ya miji ya Mbeya na Dar es salaam.

Tayari huduma katika benki hiyo zimeanza kutolewa ambapo mwandishi wa Jukwaa Huru aliyetembelea tawi hilo leo, alishuhudia baadhi ya wateja ambao wameshajiunga na huduma za benki hiyo wakiendelea kupatiwa huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo.

Ujio wa DTB jijini Mbeya, unatarajiwa kuzidi kuleta urahisi wa huduma za kibenki kwa wakazi wa eneo hili.

No comments: