Tuesday, July 26, 2011

MZEE ERNEST PAULO WAYA ASEMA SERIKALI IACHE TABIA YA KUWAONA WAMAANA WAKATI WA SIKU YA MASHUJAA IWAJALI MUDA WOTE

Mzee Ernest Paulo Waya aliyepigana vita kuu ya pili vya Dunia akiongea na Mbeya Yetu amesema serikali imewatelekeza na kutowajali kwa chochote na kuwazulumu mafao yao mashujaa hao wa zamani ila huwaona wamaana sana siku ya mashujaa na kuwaita ili washiriki pamoja siku hiyo zoezi hilo likiisha huwatelekeza mpaka mwaka mwingine tena mzee Waya amesema ndiyo maana mwaka huu wenzake wengi hawajaja wapo kujitafutia riziki maana kula yao niyashida sana

Mzee Ernest Waya akiweka upinde na mshale kuwakumbuka wenzake aliokuanao vitani enzi hizo

Shughuli imekwisha Mzee Waya huyoo ndiyo wamekwisha msahau hawana mpangonae tena

source:mbeya yetu blog

No comments: