Friday, June 3, 2011

SHAQUILLE O'NEAL ASTAAFU KIKAPU

KAMA wasemavyo watu wazima kuwa kila kilicho na mwanzo hakikosi mwisho, Hatimaye nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Shaquille Rashaun O’Neal aka Shaq aliyeisaidia timu ya Los Angeles Lakers inashiriki ligi kuu ya NBA kunyakuwa ubingwa wa mchezo huo maarufu nchini humo na ulimwenguni kote mara 3 mfululizo amestaafu rasmi.

Kwa mujibu wa ukurasa wake wa Twitter nyota huyo ambaye pia ni mkali wa kurap ametangaza kustaafu kucheza BasketBall baada ya kuutumikia dimbani kwa zaidi ya miaka 19.

Shaq alianza kucheza ligi ya NBA alipojiunga na Orlando Magic (1992-1996), Los Angeles Lakers (1196-2004),Miami Heat (2004-2008),Phoenix Suns (2008-2009),Cleveland Cavaliers (2009-2009) na mwaka Boston Celtics (2010-2011)

Mbali na kucheza BasketBall pia Shaq alikua na kipaji cha muziki mwaka 1993 kwa kutoa album yake ya kwanza ya Shaq Diesel na inasemekana kuwa kupata majeraha ya mara kwa mara huenda kumemfanya Shaq aamue kustaafu na alikua maarufu sana kwa kuvaa jezi no 32

No comments: