Friday, May 20, 2011

MWENYEKITI WA CCM RUNGWE MBEYA AUWAWA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya John Mwankenja(pichani) ameuwawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kwa kupigwa risasi usiku wakuamkia leo akiwa nje ya Nyumba yake.
Mwenyekiti huyo pia alikuwa ni diwani wa kata ya Kiwira ameuawawa kwa risasi usiku majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari baada ya kufika nyumbani kwake eneo la Kiwira
Maiti yake inapelekwa hivi sasa hospitali ya Makandana kwa kuhifadhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo kwa ujumla linaaacha maswali mengi kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe na mkoa kwa ujumla.

Chanzo cha habari hii kimeudokeza mtandao huu kuwa kada huyo wa CCM alikuwa amekodi Taxi akirejea nyumbani kwake na baada ya kufika nje ya nyumba yake alikutwa na mauti baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu hao

Habari kamili utaipata mara baada ya mwandishi wa mtandao huu kurudi eneo la tukio endelea kutembelea mtandao huu

No comments: