Thursday, May 26, 2011

MAJAMBAZI YATEKA MAGARI MLIMA KITONGA


Habari zilizotufikia usiku huu zinadai kuwa watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamefunga barabara eneo la mlima wa Kitonga na kuteka magari zaidi ya 20.

Habari zinasema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 8 hadi saa 10 usiku baada ya baadhi ya madereva kupiga simu kituo cha polisi mjini Iringa ambao walituma askari polisi wa kituo cha Ilula ambao walifika kwa wakati kunusuru usalama wa madereva ambao walikuwa wametekwa.

Mmoja kati ya madereva aliyenusurika katika tukio hilo aliueleza mtandao huu kuwa yeye alikuwa na gari jipya lenye namba za IT akitokea Dar Dar es Salaam kwenda Tunduma mkoani Mbeya akiwa na wenzake ambao walitangulia na kukumbwa na mkasa huo.


Dereva huyo alisema yeye na baadhi ya madereva walipoona hali hiyo walirudi nyuma hadi Hotel ya Kitonga hadi majira ya saa 10 usiku baada ya polisi kufika eneo hilo na kuwatawanya majambazi hayo na kuwahakikishia usalama madereva hao japo alidai kuwa usafiri wa katika barabara hiyo ulisimama kwa masaa kadhaa wakihofia kupita eneo hilo na kuwa magari yaliyotekwa ni malori na gari zenye namba za IT na gari binafsi ambazo zlikuwa zikisafiri uhusiku huo.

jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangala kwa ajili ya kupata idadi kamili ya magari yaliyotekwa na madhara yaliyojitokeza zinafanywa

Habari toka kwa :Francis Godwin ni Iringa na matukio

3 comments:

Anonymous said...

namba za IT ni nanmba gani hizo?

Anonymous said...

This info is priceless. When can I find out more?

Here is my blog post; cellulite treatment reviews

Anonymous said...

how to cure tennis elbow pain

Check out my web page :: over the counter treatment for tennis elbow