Saturday, May 28, 2011

BASI LA SUMRY LAPATA AJALI MBARALI LAUA ZAIDI YA 10

Habari iliyotua hivi punde ktk mtandao huu kutoka Igawa Mbarali mkoani Mbeya zinadai kuwa watu zaidi ya 10 wamekufa papo hapo huku wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Arusha kwenda Mbeya kupata ajali jana usiku. Maiti zimepelekwa Hospitali ya Ilembula Njombe na Hospitali ya wilaya ya Mbarali habari chanzo cha ajali hii ni kupasuka taili la mbele na mwendo kasi na kupelekea basi hilo kukosa mwelekea na kupinduka. Dereva wa basi hilo ni kati ya watu waliofariki dunia na kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 4.45 usiku. mwanahabari Dany Tweve amedai kuwa walio kufa ni wengi zaidi japo hana idadi kamili na kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo . Mtandao huu upo mbioni kufuatilia kwa kina tukio hilo na taarifa kamili utaipata hapa wakati wowote.

No comments: