
Siku chache baada ya kushindwa kutimia kwa utabiri wake Mchungaji wa kanisa moja maarufu nchini Marekani Harold Camping (89) amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa kituo cha Family Radio kilikosea mahesabu ya biblia wakati wa kutabiri mwisho wa dunia.
Akizungumza kwa kujiamini Harold alisema kulikuwa na makosa makubwa wakati wa kutangaza hesabu za kiblia alizozifanya na ukweli ni kuwa Oktoba 21 mwaka huu ndiyo itakuwa siku ya Kiama badala ya May 21 iliyokuwa imetangazwa hapo awali.
“Ni makosa ya kimahesabu yalifanyika awali lakini amini nawaambia Oktoba 21 kiama kitatokea kweli na kuua watu wote wachafu na wema watapaishwa mbinguni kuonana na Yesu” alisema Mchungaji huyo.
Katika hatua nyingine mchungaji huyo mwenye maskani yake jimboni California alisema kuwa kutotokea kwa kiama May 21 kumetokana na nguvu za kiroho na wala si nguvu za asili, na kuongeza kuwa Mungu aliwaonea huruma watu kuwaangamiza kwa matetemeko makubwa ya ardhi lakini hiyo Oktoba 21 hakutakuwa na huruma na kiama kitatokea kweli, na dunia itaangamizwa na kutoweka ndani ya muda mchache.
No comments:
Post a Comment