Ni siku nyingine ya majonzi makubwa nchini Tanzania kufuatia milipuko iliyotikisa jiji la Dar-es-salaam jana jioni.Milipuko hiyo ilitokea katika ghala la kuhifadhi silaha za kijeshi huko Gongo la Mboto.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza(BBC) kupitia idhaa yake ya Kiswahili,watu 32 wameuawa na mamia ya watu kujeruhiwa. Taarifa hiyo imemnukuu mnadhimu mkuu wa majeshi,Lt.Gen Shimbo
Mashirika mbalimbali ya habari ulimwenguni likiwemo la CNN,yameripoti kuhusu tukio hili.Hii ni mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.Mwaka 2009 zaidi ya watu 20 waliuawa na wengine 300 kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea katika ghala lingine la kijeshi katika maeneo ya Mbagala jijini Dar-es-salaam.
Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi na awaponye majeruhi wote.
No comments:
Post a Comment