BAADA ya sokomoko la juzi la Brig. Jenerali Sulaiman Mohammed Yahya Al-Adawi kukataa kupigwa picha, Jana "zimefanyika njama kinamna" dhidi yake, akapigwa picha bila kujua alipokuwa anatembelea mitambo yake ya Dowans Ubungo, Dar es Salaam. Ndiye huyu hapa! Na baada tu ya ziara yake hiyo, akaelekea uwanja wa ndege kupanda pia kurudi makwao Oman. Hata hivyo, kabla ya tukio hilo la Ubungo, Adawi alimtembelea Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal, Ikulu, na akiwa ofisini kwa mamaku wa rais, alikataa katakata kupigwa picha yoyote kama alivyowagomea waandishi juzi.
Alivyokutana na waandishi, alisema amekuja kujadiliana na Tanesco juu ya hatima bora ya kibiashara kwake na fursa ya umeme kwa Watanzania, katika mazingira ya sasa ya mkataba unaodaiwa kuwa na utata, na deni la bilioni 94 analoidai Tanesco baada ya Dowans kuwashinda Tanesco mahakamani. Alizungumza kwa Kiingereza, na nimeweza kunukuu baadhi ya kauli zake moja kwa moja alipokuwa akijibu baadhi ya maswali na hoja za waandishi. Hizi hapa:
1. “I am here to find a happy resolution, a business decision. I am ready to offer something nice to Tanesco if it works out.”
2. “I don’t want to be known. I am a low-profile businessman. I walk free here in Dar es Salaam, and no one knows I own Dowans.”
3. “Rostam Azizi is a friend of mine. He invited me to come and invest here, but he didn’t put in any cent in the project.”
4. “I have businesses in 12 countries allover the world. I can’t go and represent myself in every country. That’s why I gave Rostam power of attorney.”
5. “We have not been tarnished, but we have been mixed up with something else (Richmond)”
6. “I do not need to be cleared by anyone; my electricity here will clear me.”
source:ngurumo blog
No comments:
Post a Comment