
Hali ya wasiwasi imewakumba wakazi wa kijiji cha Gibasu wilayani Tarime kufuatia kupotea kwa vijana sita ambao wanadaiwa waliingia kwenye Hifadhi ya Serengeti eneo la Lamai kwa ajili ya kuwinda na kuwa huenda walikurupushwa na askari wanyamapori wanaotuhumiwa kuwafyatulia risasi.
Tobias Chacha ni kijana aliyenusurika katika tukio hilo amedai kuwa baada ya kuingia katika hifadhi hiyo walikurupushwa na askari wa wanyamapori ambao walikuwa wanafyatua risasi ambapo vijana Watano kati ya 11walipotea.
Katika tukio hilo lililotokea zaidi ya mwezi mmoja sasa,vijana hao wanadaiwa kuingia katika hifadhi ya Serengeti eneo la Lamai wilayani Tarime na kupotea baada ya kukurupushwa na askari wanyamapori huku wazazi wa vijana wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua kama vijana wao wamekufa au wapo hai kwa sababu mrefu umepita bila vijana hao kuonekana.
Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya Cosntantine Massawe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kuwa uchunguzi unaendelea ingawa hadi sasa ni mwezi mmoja umepita na hakuna taarifa yeyote inayowahusu vijana hao.
Wananchi wa kijiji cha Gibaso ombi lao kubwa ni kupatikana kwa vijana wao ili hofu yakuwa wamekufa iwaondoke.
Emmanuel Amas TBC Tarime
No comments:
Post a Comment