Tuesday, December 21, 2010

BREAKINGNEWS............BAADA YA MITAKA MITATU POLISI WAMTIA MBARONI DEREVA WA AJALI ILIYOPELEKEA KIFO CHA WAZIRI SALOME MBATIA


HATIMAYE baada ya kupita miaka mitatu na miezi miwili kutoka gari lenye namba za usajili T 724 AGZ Nissan Patrol alilokuwa akitumia aliyekuwa naibu waziri wanawake ,jinsia na watoto marehemu Salome Mbatia kugongwa na fuso na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wawili ,jeshi la polisi mkoani Iringa limefanikiwa kumkamata dereva wa fuso lililosababisha kifo cha naibu waziri huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla ameueleza mtandao huu leo kuwa dereva huyo wa Fuso lenye namba T 299 AFJ ,Daud Mangulla (28) (pichani)mkazi wa mjimwema makambako wilaya ya Njombe alikamatwa jana akiwa stendi ya mabasi ya makambako .


Alisema kuwa kukamatwa kwa dereva huyo kumetokana na msaada mkubwa ulioonyeshwa na wananchi kupitia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa jeshi hilo la polisi.

Kamanda Mangalla alisema kuwa tokea ajali hiyo itokee Octoba 24 mwaka 2007 majira ya saa 10.50 jioni eneo la Kibena barabara kuu ya Njombe -Makambako , jeshi la polisi lilikuwa likiendelea kumsaka dereva huyo ambaye alitoweka baada ya ajali hiyo.

Mangalla aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na dereva wa gari ya naibu waziri huyo Anakleti Mbogela (42) na utingo wa Fuso hilo Castory Kulangwa (22) huku majeruhi walikuwa ni NIcolaus Lubava (33) na Dastan Ngonza (26).

Alisema kuwa dereva huyo alikuwa amejificha porini na baada ya kuona mambo yamekuwa kimya ndipo alipoamua kujitokeza na kuendelea na shughuli zake za kila siku eneo la mjimwema Makambako.hivyo alisema jeshi la polisi litamfikisha mahakamani dereva huyo wakati wowote kuanzia sasa.
Kwa upande wake dereva huyo alipohojiwa na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com alidai kuwa baada ya ajali alijificha katika msitu wa kibena uliokuwa jirani na eneo hilo la ajali kuanzia majira ya saa 10 jioni hadi saa 2 usiku ambapo alitoka na kutafuta usafiri na kwenda kulala nyumbani kwake mji mwema Makambako .
Mangulla amesema kuwa kwa muda wote alikuwa akijificha katika misitu mbali mbali huku chakula akitegemea kutoka katika familia yake .

No comments: