Wednesday, November 10, 2010

JK atoa tangazo la kuitisha Bunge


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. JAKAYA KIKWETE ametoa rasmi tangazo la kuitisha bunge la Kumi kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika nchini kote tarehe Thelathini na Moja mwezi huu na kuanza kwa utawala mpya.

Katibu wa Bunge Dkt. THOMAS KASHILILA ameitisha mkutano na waandishi wa habari jijiini DSM hii leo na kuwasomea ratiba ya mkutano wa kwanza wa bunge hilo la KUMI utakaoanza tarehe Kumi na Mbili hadi Kumi na Saba mwezi huu.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo wabunge wanatakiwa kuwasili DODOMA kwa ajili ya usajili kuanzia kesho ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA atatoa hotuba ya kuzindua bunge tarehe Kumi na Saba mwezi huu saa Kumi jioni.

No comments: